180 – Pana Mahali Pazuri Mno

( 428 – Sweet By and By )

1. Pana mahali pazuri mno,
Twapaona kwa mbali sasa;
Baba yetu angoja pale,
Amepanga makao yetu.

Kitambo tu bado,
Tutakutana ng’ambo pale.
Kitambo tu bado,
Tutakutana ng’ambo pale.

2. Tutaimba pale kwa moyo
Nyimbo tamu za wenye heri.
Na rohoni hatutaona
Tena haja ya kupumzika.

3. Kwa Baba yetu mkarimu
Tutatoa shukrani sana,
Kwa kipaji cha pendo lake
Na baraka anazotupa.

WhatsApp
Listen to Mbarikiwa Radio

Instagram

Twitter

Recent Comments