1. Raha yangu yote, Bwana, I mbavuni pako;
Mimi sina haja tena ila kifo chako.
2. Mwokozi uliyekufa, nawe ndiwe Mungu,
Kifo chako ni kwa dhambi, ziondoe zangu.
3. Nioshe na niwe wako, nawe uwe wangu;
Nioshe damuni mwako liwe fungu langu.
4. Nioshe si miguu tu, osha tangu nyayo,
Hata kichwa changu juu, na ndani ya moyo,
5. Na iwe kafara damu nifanyapo kazi,
Hata imani itimu, nikwone,Mwokozi.