1. Mfalme yu mlangoni, Ndiye aliyetufia;
Mara wote wampendao atawakusanya.
Yuaja, yuaja, mlangoni anasimama;
Anakuja, anakuja, Kuja kwake karibu.
2. Dalili za kuja kwake Zinazidi kutimizwa;
Karibu wateule watamlaki Bwana.
3. ‘Sitafute duniani amani wala furaha,
Mpaka Bwana arudi dhambi kuondoa.
4. Tutakaa na Mwokozi Makaoni ya milele;
Daima tutafurahi kuwa watu wake.