1. Huniongoza Mwokozi, ndipo nami hufurahi,
Niendapo pote napo, ataniongoza papo.
Kuongoza hunishika; kwa mkono wa hakika;
Nitaandamana naye Kristo aniongozae.
2. Pengine ni mashakani nami pengine rahani;
Ni radhi, ijayo yote, yupo nami siku zote.
3. Mkono akinishika kamwe sitanung’unika;
Atakachoniletea ni tayari kupokea.
4. Nikiisha kazi chini sita kimbia mauti;
Kushinda ni ya hakika nikiongozwa na Baba.