1. Mchungaji mpenzi hukuita uje
Katika zizi lake Panapo salama;
Akina wanawake, waume vijana,
Yesu aliye kweli, huwaita kwake
Huita kwa moyo wa huruma, ‘Uluyepotea uje kwangu’;
Hivi kukungoja anadumu Bwana Yesu Mchunga.
2. Akatoa maisha kwa ajili yetu;
Ataka wapotevu waje kwake sasa;
Tusijihatirishe; Kwake tu salama;
Sikia wito wake, Mchungaji wetu.
3. Tusikawie tena, adui shetani,
Kama Mbwa wa mwitu, atatuharibu;
Tunaitwa na Yesu, Mkombozi wetu,
Tuingie zizini, panapo nafasi.