1. Nataka Imani hii: Imani imara
Ambayo haitetemi Kitu chote Wakati wa shida,
Wakati wa shida.
2. Isiyonung’unika Huzuni, taabu;
Lakini katika saa ya matata Humwamini Mungu,
Humwamini Mungu.
3. Imani inayo ng’aa katika tufani;
Isiyoogopa giza, wala shida, Njaa na Hatari,
Njaa na hatari.
4. Haiogopi dunia, Kudharau kwake;
Haiangushwi na hila, na uwongo Dhambi na ogofyo,
Dhambi na ogofyo.
5. Bwana, nipe imani hii, Hivi nita weza
Kuonja hapa chini ulimwenguni, Kurithi furaha,
Kurithi furaha.