77 – Habari Za Usiku

( 601 – Watchmen, on the Walls of Zion )

1. Je! Mkinzi ukutani
Wa mji wa Zayuni,
Habari zake usiku?
Asubuhi karibu?
Kuna dalili za kupambazuka?
Kuna dalili za kupambazuka?

2. Katika safari yetu
Twaona nchi kavu?
Tutalala baharini?
Bandari bado mbali?
Kweli, kweli tutaona ufalme?
Kweli, kweli tutaona ufalme?

3. Tunaona nuru yake
Nyota ya asubuhi;
Nyota, tukufu na safi
Inang’aa mbinguni;
Furahini, wokovu u karibu.
Furahini, wokovu u karibu.

4. Tumetazama ramani,
Kweli pwani si mbali;
Twende mbele, kwa upesi
Tutaona bandari;
Furahini, imbeni nyimbo zenu.
Furahini, imbeni nyimbo zenu.

WhatsApp
Listen to Mbarikiwa Radio

Instagram

Twitter

Recent Comments