1. Mrithi ufalme kwani walala?
Karibu wokovu wasinzia?
Amka simama uvae silaha
Haraka sana saa zapita.
2. Mrithi ufalme mbona ‘kawia’?
M-bona hupokei zawadi?
Haya uvae, Mwokozi yuaja;
Haraka, umlaki apitapo.
3. Mataifa makuu ya dunia
Yapigana na kujiangusha.
Usiziofu dalili, Mrithi;
Ishara zotte hazikawii.
4. ‘Sitazame anasa za dunia!
Kwani hayo ya pita upesi.
Zivunje kamba zinazokufunga.
Mrithi ufalme, njoo’karudi.
5. Inua kichwa, tazama mbele tu.
M-falme aja na utukufu;
Jua la onekana milimani,
Warithi ufalme furahini.