1. Msingi imara, ninyi wa Bwana,
Ume wekwa kwenu kwa neno lake?
Nini zaidi atasema Bwana?
Imani yenu ipate kuzidi?
2. Wanbiwapo vuka maji ya giza,
Mito ya mashaka haitazidi;
‘Takuwapo nawe, nikuwezeshe,
Shida upatazo zisikutishe!
3. Utakapopishwa Ndani ya moto
Nguvu nitakupa, upate pato;
Huteketezwi, ila taka zako.
Na zitasalia dhahabu zako.
4. Na mtu aliyenitegemea
Nguvu za jehanamu zijapotisha,
Kamwe kwa adui sitamtia;
Mtu wangu kamwe sitamuacha.