1. Ninaye rafiki naye Alinipenda mbele;
Kwa kamba za pendo lake Nemefungwa milele:
Aukaza moyo wangu, Uache ugeuzi,
Ninakaa ndani yake, Yeye kwangu milele.
2. Ninaye Rafiki ndiye Aliyenifilia;
Alimwaga damu yake kwa watu wote pia;
Sina kitu mimi tena, Nikiwa navyo tele;
Pia vyote ni amana Ndimi wake milele.
3. Ninaye Rafiki naye Uwezo amepewa;
Atanilinda mwenyewe, Juu ‘tachukuliwa;
Nikitazama mbinguni Hupata nguvu tele;
Sasa natumika chini, Kisha juu milele.
4. Ninaye Rafiki naye Yuna na moyo mwema,
Ni Mwalimu Kiongozi, Mlinzi wa daima;
Ni nani wa kunitenga, Na mpenzi wa mbele?
Kwake nimetia nanga, Ndimi wake milele.