1. Ewe roho wa mbinguni, Maombi sikia!
Makao yako yafanye Mioyoni mwetu.
2. Kama nuru, tupenyeze, Giza uondoe;
Siri yako tuone, Na amani yako.
3. Kama moto, tusafishe, Choma dhambi yetu;
Roho zetu ziwe zote Hekalu la Bwana.
4. Kama umande, na uje, Utuburudishe,
Moyo ‘kavu utakuwa Ni wenye baraka.
5. Kaka upepo Ee Roho, Katika Pentekoste
Ukombozi Utangaze, Kwa kila taife.