1. Nasifu shani ya Mungu, mweneza bahari,
Muumba pia wa mbingu, jua, nyota, mwezi.
Ni tukufu yako shani, mtengeza mambo
Ya nyakati na zamani, yasiyo na mwisho.
2. Kadiri ya nionayo, yakusifu Mungu;
Nchi niikanyagayo, na hayo mawingu;
Hakuna hata unyasi, usiokukuza;
Na upepo wavumisha, au kutuliza.
3. Nami kwa mkono wako, naongozwa sawa,
Ni pato nikusipo, kukwomba ni dawa;
Umenizingira nyuma, na mbele baraka,
Maarifa ya ajabu! Yanishinda mimi!