37 – Pendo Lako, Ee Mwokozi

( 191 – Love Divine )

1. Pendo lako, Ee Mwokozi, Hushinda pendo zote!
Kaa nasi, ndani yetu, Furaha ya mbinguni.
Yesu u rehema tupu, Safi na Kusamehe,
Mfariji mwenye huzuni Ziondoe machozi.

2. Roho yako ya upendo, Tuma kwa kundi lako;
Hebu tuirithi raha, Iliyoahidiwa,
Uondoe moyo mbaya, U Mwanzo tena Mwisho;
Timiza imani yetu, Ili tuwekwe ‘huru.

3. Yesu, uje kwetu sasa, Tupokee huruma;
Rudi kwetu, tena kamwe Usituache pekee,
Tungekutukuza leo, Pamoja na malaika,
Imba na kutoa sifa, Ingia kwa ibada.

4. Sasa, Bwana, kazi yako, Imalize moyoni;
Takasa hekalu lako, Wokovu kamilisha!
Safisha viumbe nyako Katika wakati huu;
Tupumzike ‘toka dhambi, Tuingie mbinguni.

WhatsApp
Listen to Mbarikiwa Radio

Instagram

Twitter

Recent Comments