35 – Nimekombolewa Na Yesu

( 337 – Redeemed! )

1. Nimekombolewa na Yesu na sasa nimefurahi;
Kwa bei ya mauti yake mimi ni mtoto wake.

Kombolewa! Nakombolewa na damu.
Kombolewa! Mimi mwana wake kweli.

2. Kukombolewa nafurahi, Kupita lugha kutamka;
Kulionyesha pendo lake, mimi ni mtoto wake.

3. Nitamwona mfalme wangu katika uzuri wake,
Ambaye najifurahisha katika torati yake.

4. Najua taji imewekwa mbinguni tayari kwangu,
Muda kitambo atakuja ili alipo niwepo.

WhatsApp
Listen to Mbarikiwa Radio

Instagram

Twitter

Recent Comments