1.Tena, Mwokozi, twalitukuza
Jina lako lenye kupendeza,
Twangojea neno la amani,
Kabla hatujakwenda nyumbani.
2.Tupe amani njiani mwetu,
Wewe u mwanzo, u mwisho wetu;
Dhambini kamwe isiingie
Midomo ikitajayo wewe.
3.Utupe amani usiku huu,
Ili gizani kuwe nuru kuu.
Tulinde kwa kuwa kwako Bwana.
Usiku ni sawa na mchana.
4.Tupe amani ulimwenguni
Ndiyo dawa yetu majonzini;
Na ikitwita sauti yako,
Tupe amani milele kwako.