1. Jina lake Yesu tamu Tukilisikia,
Hutupoza, tena hamu Hutuondolea.
2. Roho ilioumia Kwalo hutibika,
Chakula, njaani pia; Raha, tukichoka.
3. Jina hili ni msingi, Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata ungi, Kwangu ni akiba.
4. Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, mwisho, na amina, mali yangu yote!