1. Ahadi tamu kwa waamini, Tazama nakuja upesi sana.
Uwe imara, hatari kubwa: Ndugu usilale, bali ukeshe.
Uihifadhi imani yako,–Dunia mpya itatolewa
Njoo ingia furaha yangu; Taji zinangoja; Uwe imara.
2. Tatakesha na kutoa sala; Atakuja kama mwivi kwa wengi;
Ya kwamba yu karibu twajua, Ila hatujui ni siku gani.
3. Tunategemea Neno lake, Ambalo latangaza kuja kwake,
Tumaini letu ni ahadi: “naja karibuni, uwe imara.”