1. Sijui atakapokuja, Mchana au usiku;
Labda sa-a ya alasiri, Pengine ni alfajiri.
Hutwambia tuwe tayari, Ta-a zetu tusizime;
Ili ajapo atukute; Tuwe tukimngoja Yeye.
Tu – – – kimngojea – – – a,
(kukesha, tunakungoja Wewe)
Tu – – – kimngojea – – – a,
(kukesha, tunakungoja Wewe)
Tu – – – kimngojea – – – a,
(kukesha, tunakungoja Wewe)
Twakesha, twamngoja Yeye.
2. Nakumbuka huruma zake, Bei ya wokovu wetu:
Aliacha nyumba tukufu, Awafilie wabaya.
Ninadhani itampendeza, Kama sisi watu wake,
Tukionyesha pendo letu, Tuwe tukimngoja Yeye
3. Ee Yesu, Mwokozi mpendwa, Wajua nalihifadhi.
Tumaini la kukuona. La kukaribishwa nawe.
Ukija kwa watu wengine, Kama mhukumu wao,
Kwangu utakuwa rafiki,–Nakesha, nakungojea.