1. Mchana hauishi Mjini mzuri;
Mji hautapita; Na hapana giza.
Machozi yatafutwa, Kifo hapana pale;
Hawahesabu siku, Na hapana giza.
2. Milango ni ya lulu, Mjini mzuri;
Dhahabu njia zake; Na hapana giza.
3. Milango haifungwi Mjini mzuri;
Mto ni wa uzima Na hapana giza.
4. Hawahitaji jua Mjini mzuri, Mwana Kondoo nuru;
Na hapana giza.