184 – Panapo Pendo

( 652 – Love at Home )

1. Vitu vyote ni sawa, panapo pendo; Kila sauti tamu, panapo pendo.
Pana amani pale, na furaha nyumbani, Siku zote salama, panapo pendo.

Panapo upendo Siku zote salama,
Panapo pendo

2. Furaha I nyumbani, panapo pendo; Hapana machukizo, panapo pendo;
Chakula ni kitamu, mashamba yasitawi, Maisha ni kamili, panapo pendo.

3. Hata mbinguni juu, pana furaha Wakiona upendo nyumbani mwetu.
Macho yanapendezwa na viumbe vya Mungu, Naye Mungu huona, panapo pendo.

3. Ee Yesu niwe wako, wako kabisa, Ndipo patakuwako Pendo nyumbani;
Nitakaa salama, sitaifanya dhambi; Nitabarikiwa tu panapo pendo.

WhatsApp
Listen to Mbarikiwa Radio

Instagram

Twitter

Recent Comments