1. Mwamba wenye imara, kwako nitajificha!
maji hayo na damu, yaliyotoka humu,
hunisafi na dhambi, hunifanya mshindi
2. Kwa kazi zote pia , sitimizi sheria.
nijapofanya bidii, nikilia nakudhii,
hayaishi makosa: Ndiwe wa kuokoa.
3. Sina cha mkononi, Naja Msalabani;
Nili tupu, nivike; Ni mnyonge, nishike;
Nili mchafu naja, Nioshe nisijafa.
4. Nikungojapo chini, nakwenda kaburini;
nipaapo Mbinguni, na kukwona enzini;
roho yangu na iwe rahani mwako wewe.