1. Twaomba, Bwana, umpokee Kama mhudumu;
Ambaye anjitoa Kuwa mtumishi.
2. Twaomba, Bwana, umpokee Kama mhudumu;
Neno lako alitoe, Mwangaza kung’aa.
3. Mwokozi wetu, twaomba, na umwandikie
Kitabuni mwako juu Mjumbe wa injili.
4. Silaha zake apewe Kumshinda adui;
Vitabuni awe hohari, Mpaka mauti.
5. Yeye ashindaye, Bwana, Kwa rehema yako,
Ile taji ya dhahabu, Nawe utampa.