1. Kitambo Bwana yuaja, atafute kote
Vito vya thamani kubwa: mali yake kuu.
Kama nyota tajini vitang’aa sana, Vito vizuri kweli vyenye thamani.
2. Karibu atakusanya vito kwa ufalme,
Vizuri vinavyong’aa: mali yake kuu.
3. Watoto wote wadogo wampendao Yesu,
Ndiyo vito ving’aavyo: mali yake kuu,