1. Anipenda ni kweli: Mungu anena hili;
Sisi wake watoto kutulinda si zito.
Yesu Mwokozi ananipenda; Kweli hupenda, Mungu amesema.
2. Kwa kupenda akafa niokoke na kufa:
Atazisafi taka sana ataniweka.
3. Anipenda kabisa; niuguapo sasa,
Anitunza mbinguni niliyelala chini.
4. Kunipenda haachi tu sote hapa chini,
Baada ya mashaka kwake tanipeleka.