23 – Yesu Furaha Ya Moyo

( 242 – Jesus, Thou Joy of Loving Hearts )

1. Yesu, furaha ya moyo! Hazina ya pendo, na nuru.
Yote yatupendezayo, yasilinganishe nawe.

2. Kweli yako ya daima, wawajibu wakwitao,
Ni siku zote u mwema kwao wakutafutao,.

3. U mkate wa Uzima, kupokea ni baraka,
Twanya kwako u kisima roho zikiburudika.

4. Mwokozi twakutamani, kwako roho hutulia;
Twakushika kwa imani, nawe watubarikia.

5. Yesu, ndiwe kwetu mwanga, tufurahishe daima;
Giza ya dhambi fukuza, uwe mwanga wa Uzima.

WhatsApp
Listen to Mbarikiwa Radio

Instagram

Twitter

Recent Comments