28 – Jina La Thamani

( 474 – Take the Name of Jesus With You )

1.Jina lake Yesu tamu, Lihifadhi moyoni;
Litatufariji ndugu, Enda nalo po pote.

Jina la (Thamani) thamani, (thamani)
Tumai la dunia
Jina la (Jina la thamani-tamu!) thamani,
Furaha ya mbinguni.

2.Jina la Yesu lafaa Kama ngao vitani,
Majaribu yakisonga, Omba kwa jina hili.

3.Jina hili la thamani Linatufurahisha,
Anapotukaribisha, Na tunapomwimbia.

4.Mwisho wa safari yetu Tutakapomsujudu,
Jina hili tutasifu Furaha ya mbinguni.

WhatsApp
Listen to Mbarikiwa Radio

Instagram

Twitter

Recent Comments