1.Yesu nakupenda, U mali yangu,
Anasa za dhambi sitaki kwangu;
Na mwokozi aliyeniokoa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
2.Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
3.Ulipoangikwa Msalabani
Tusamehewe tulio ndambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.
4.Mawanda mazuri na masikani
Niyatazamapo huko mbinguni,
‘Tusema na taji nitakayovaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.