(
341 – To God Be the Glory )
- Mungu atukuzwe, kwa mambo makuu,
Upendo wake ulitupa yesu,
Aliyejitoa maisha yake,
Tuwe nao uzima wa milele.
Msifu, msifu dunia sikia;
Msifu, msifu, watuwafurahi;
Na uje kwa baba, kwa yesu mwana
Ukamtukuze kwa mambo yote
- Wokovu kamili zawadi kwetu,
Ahadi ya mungu kwa ulimwengu;
Wanaomwamini na kuungama,
Mara moja wele husamehewa.
- Alitufundisha mambo makuu,
Alihakikisha wokovu wetu;
Lakini zaidi ajabu kubwa,
Yesu atakuja na tutamwona.