1.Yesu unipendaye kwako nakimbilia,
Ni wewe utoshaye mwovu akinijia.
Yafiche ubavuni mwako maisha yangu;
Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu.
2.Ngome nyingine sina; nategemea kwako,
Usinitupe Bwana, nipe neema yako,
Ninakuamania, mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia, vitani wanitosha.
3.Nakutaka Mpaji, vyote napata kwako;
Niwapo muhitaji, utanijazi vyako;
Nao waangukao wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao, uongoze vipofu.
4.Mwana umeniosha moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona kisima cha uzima;
Mwangu moyoni, Bwana, bubujika daima.