1. Niimbe (niimbe) pendo lake,
Pendo la (pendo la) Yesu Bwana;
Sababu (sababu) alitika
Kwa Baba akafa.
Niimbe (niimbe) pendo lake;
Sifa kuu (sifa kuu) nitatoa;
Akafa (akafa) niwe hai, —
Niimbe pendo lake.
2. Machozi (machozi) alitoa
Ijapo (ijapo) sijalia;
Maombi (maombi) yangu bado,
Aniombeapo.
3. Upendo (upendo) kubwa huo!
Dunia (dunia) haijui
Samaha (samaha) kwa makosa
Kubwa kama yangu.
4. Hapana (hapana) tendo jema
Ambalo (ambalo) nilitenda,
Nataka (nataka) toka leo
Nimwonyeshe pendo.