1. Nipe habari za Yesu, Kwangu ni tamu sana:
Kisa chake cha thamani Hunipendeza sana.
Jinsi malaika wengi walivyo imba sifa,
Alopoleta amani kwa watu wa dunia.
Nipe habari za Yesu, Kaza moyoni mwangu;
Kisa chake cha thamani Hunipendeza sana.
2. Kisa cha alivyogungwa Peke yake jangwani.
Jinsi alivyomshinda Jaribu la Shetani;
Kazi aliyoifanya, Na siku za huzuni,
Jinsi walivyomtesa: Yote ni ya ajabu!
3. Habari za Msalaba Alivyosulubiwa;
Jinsi walivyo mzika, Akashida kaburi.
Kisa chake cha rehema. Upendo wake kwangu.
Alivyotoa maisha Nipokee wokovu.