1. Njoo, Roho Mtukufu uoshe moyo wangu,
Utakase nia yangu, njoo, nijaze sasa.
Roho Mtukufu, njoo, nijaze sasa;
Utakase nia yangu, njoo, nijaze sasa.
2. Unijaze moyo wangu Ijapo sikuoni,
Nami ninakuhitaji, njoo, nijaze sasa.
3. Nimejaa udhaifu, nainamia kwako;
Roho Mtukufu sasa, nitilie na nguvu.
4. Unioshe nifariji niponye, nibariki,
Unijaze moyo wangu; ndiwe mwenye uwezo.