1. Miguuni pake Yesu, Maneno yake tamu;
Pahali palipo heri, Niwepo kila siku,
Miguuni pake Yesu Nakumbuka Upendo
Na hisani vyake kwangu, Vimenivuta moyo.
2. Miguuni pake Yesu, Hapa pahali bora
Pakuweka dhambi zangu: Pahali pa pumziko.
Miguuni pake Yesu, Hapa nafanya sala,
Kwake napewa uwezo, Faraja na neema.
3. Unibariki Mwokozi, Ni miguuni pako,
Unitazame kwa pendo, Nione uso wako.
Nipe Bwana nia yake Ili ionekane
Nimekaa na Mwokozi Aliye haki yangu.