1. Ni heri kifungo kinachotufunga
Mioyo yetu kwa pendo la Kikristo.
2. M-bele ya Baba Tunatoa sala,
Hofu, nia masumbufu Yetu ni mamoja.
3. Tunavishiriki Matata na shida,
Na mara nyingi twatoa Chozi la fanaka.
4. Tunapoachana Moyoni twalia;
Lakini tutakutana M-wisho mbinguni.