5 – Na Tumwabudu Mfalme Mtukufu

( 083 – O Worship the King )

  1. Natumwabudu huyo Mfalme,Sifa za nguvu zake zivume;
    Ni ngao ni ngome Yeye milele,
    Ndizo sifa zake kale na kale.
  1. Tazameni ulimwengu huu,Uliyoumbwa ajabu kuu;
    Sasa umewekwa pahali pake,
    Hata utimize majira yake.
  1. Kwa ulinzi wako kwetu Bwana,Twakushukuru U mwema sana;
    Hupewa chakula kila kiumbe,
    Kila kitu kina mahali pake.
  1. Wanadamu tu wanyonge sana,Twakutumaini Wewe Bwana;
    Kamwe haupungui wako wema,
    Mkombozi wetu Rafiki mwema.
WhatsApp
Listen to Mbarikiwa Radio

Instagram

Twitter

Recent Comments