1. Nakaza mwendo mbinguni, kila siku napanda juu;
Naomba nikisafiri, “Bwana uniongoze juu.
Bwana uniinue juu Kwa imani hata mbingu,
Juu kuliko dunia; Bwana uniongoze juu.
2. Moyo wangu hutaki Kukaa palipo shaka;
Wengine wapenda chini nia yangu ni ku panda.
3. Nataka kupanda juu Nisishindwe na adui;
Kwa imani nasikia sauti ya washindaji.
4. Kupanda juu nataka niuone utukufu;
Hata mwisho nitaomba, “Bwana uniongoze juu.”