1. Niambie, Ee mlinzi, Umepambazuka je!
Utukufu wa Zayuni; Pana dalili zake?
Msafiri uondoke, Utazame mbinguni,
Kiunoni ujifunge, Ni kucha, alifajiri.
2. Mlinzi, inamurika nuru njiani mwako,
Dalili ya kuja kwake, Kwamba siku karibu;
Panda itakapolia Itawaamsha wafu,
Watakatifu wa Mungu, Kuwapa kutokufa.
3. Mlinzi, ione nuru Ya mwaka wa Sabato;
Sauti zina tangaza Ufalme ni karibu:
Msafiri ninaona mlima wa Zayuini,
Mji wa Yerusalemu nayo fahari yake.
4. Kwenye mji wa dhahabu Anaketi Mfalme
Katika kiti kizuri: Huku ana tawala.
Pana amani po pote, Mashamba husitawi;
Na srdhi ina rutuba; Mito ni mitulivu.
5. Mlinzi, twakaribia Nchi iliyo nzuri;
Twende mbele, tufurahi, Nchi inachangamka.
Sikieni kuna wimbo Wa waliookoka;
Kaza mwendo, Ujiunge na kundi kubwa hili.