1. Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru;
Nasi twaona raha, Kuja kushukuru;
Leo watu wa Mungu, wadogo, wakubwa,
Hukaribia mbingu, lilipo baraka.
2. Leo, ndiyo bandari, nasi twawasili,
Hiyo bustani nzuri, ya nyingi fadhili:
Kijito cha baridi kimefanya ziwa,
Na kiu ikizidi, twanywa maridhawa.
3. Leo ngazi na iwe ifakayo juu,
Mawazo na yasiwe ya duniani tu;
Leo ni kujilisha chakula cha mbingu,
Na kujifurahisha kwa mambo ya Mungu.